Waislamu wa Nakuru, wafuasi wa Ahlul-Bayt, walikusanyika katika Ijumaa ya kwanza ya Ramadhan kwa upendo na mshikamano, wakisherehekea kuingia Mwezi wa: Toba, Rehema na Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia ibada mbalimbali.

23 Februari 2026 - 22:11

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Nchini Kenya, katika mji wa Nakuru, Waislamu ambao ni wafuasi wa Ahlul-Bayt walikusanyika kwa upendo wa kiudugu katika Siku ya Ijumaa ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Walifurahia kuingia pamoja katika ibada hii tukufu ya Funga Ramadhan, tukikumbuka kwamba mwezi huu ni fursa adhimu na ya kipekee ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Subhana wa Ta’ala) kupitia sala, dua, Qur’ani, na ibada nyingine mbalimbali.

Mwenyezi Mungu Anasema katika Qur’ani:


"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ"


(Sura Al-Baqarah, Aya 183)

"Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga Ramadhani kama walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuwa (na Taq'wa) Wacha Mungu."
Rasulullah (s.a.w.w) alisema:


"مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ"


"Yeyote atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutegemea thawabu, atasamehewa dhambi zake za awali (alizozitanguliza)."
Hivyo basi, Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni muda wa toba, kutafuta msamaha, na kufanya ibada mbalimbali kwa moyo safi, kwa ajili ya kujikarabati kiroho na kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu (swt), pamoja na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu kati ya wafuasi wa Ahlul-Bayt na Waislamu wote duniani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha